Kupitia ushahidi huu, Prince Jackson, Mtoto wa Michael Jackson aamsha upya hisia za watu kuhusiana na Daktari Conrad Murray kwa kifo cha Michael Jackson.


Paris na Prince Jackson - Watoto wa Michael Jackson
Mtoto wa Michael Jackson, Prince jackson naye amepanda kizimbani kutoa ushahidi wake katika kesi mpya inayoendelea sasa ya Kifo cha Michael dhidi ya kampuni ya AEG Live ambayo ndiyo ilikuwa inaandaa onyesho lake la mwisho, ambapo ushahidi wake umemlenga tena Dr. Conrad Murray na kugusa hisia za wengi pale mtoto huyu alipoelezea namna daktari huyu alivyowafikishia habari za kifo cha baba yao.



Prince Jackson amesema kuwa, anakumbuka siku ya kifo cha baba yake, alikuwa ameketi sebuleni katika jumba lao la Hombly Hills wakati ambapo baba yao alizidiwa, na ndipo alipoanza kusikia kelele, na Daktari huyu alimwita chumbani alipokuwa Michael wakati akijaribu kumfanyia huduma za mwisho na mwisho wa siku katika hali ya kutokujali, Daktari huyu aliwaeleza moja kwa moja kuwa baba yao tayari amekufa ['Sorry Kids. Dad's Dead.'].
Maelezo haya yamegusa kwa kiasi kikubwa hisia za Daktari huyu (Conrad Murray) ambaye mpaka sasa anatumikia kifungo kwa makosa ya kusababisha kifo cha Michael.

Dr Conrad Murray
Prince pia ameweka wazi ni kwa jinsi gani kifo cha baba yao kilivyomuathiri kwa kiasi kikubwa mdogo wake, Paris ambaye mpaka sasa yupo katika kipindi kigumu kukabiliana na hali halisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post