MSHINDI WA DROO YA PILI KAMPENI YA WINDA NA USHINDE ATANGAZWA.



  
 Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo (wa pili kulia) akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde  Mwl.Michael Valerian Mbuya katika mkutano na wana habari uliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Meneja mauzo  wa Push Mobile Rugambo Rodney, kulia kwake ni Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Humudi Abdul Hussen(wa kwanza kushoto).
 Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo(katikati) akiongea na wana habari wakati wa kumtangaza mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde katika mkutano uliofanyikajana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam. 
 Wakihakiki namba za simu za mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde iliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti, wa kwanza kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo, Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko(katikati) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Humudi Abdul Hussen(kushoto).

*************
Mshindi asherekea kitita cha 1,000,000 huku akiwapongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa promosheni hiyo. 

25 Juni 2013, kampuni ya bia ya Serengeti imetangaza mshindi wa pili wa kampeni ya Winda na Ushinde ambae amejinyakulia kitita cha milioni moja baada ya kuchezesha droo yake ya pili. Droo hiyo ilichezeshwa katika ofisi za kiwanda hicho jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mhakiki kutoka katika bodi ya uchezeshaji promosheni bwana Humud Abdul Hussein.

Baada ya kupokea Michael Varelian Mbuya (29) ambae ni mwalimu wa sekondari kutoka Tabata Dar es salaam alionesha furaha yake na kubaki bumbuwazi kwa furaha. “Nina furaha isiyokifani kuwa mshindi wa promosheni hii ya Winda na Ushinde kutoka katika kampuni ya bia Serengeti na ntaitumia kufungua duka kwani ni ndoto yangu kubwa. Na najivunia kuitumia bia ya serengeti kwani ndio bia niipendayo na nawapongeza sana kampuni ya Serengeti kwa kuanzisha mashindayo haya na mpaka sasa nimeshajishindia bia nyingi pamoja na bia taslimu” alisema mshindi huyo.

Akiongelea promosheni hii meneja wa kinywaji cha Serengeti Mr.  Allan Chonjo alisema “promosheni hii ni ya kipekee na mpaka sasa watu 110,000 wameshajishindia bia za bure na pesa taslimu ambazo ni shilingi 10,000 na100, 000/= na droo ya kwanza ilichezeshwa mwezi uliopita huku mshindi kutoka Moshi akiondoka na kitita cha milioni moja, pia promosheni hii inampa fursa mshindi kununua kile anachokitaka baada ya kujishindia fedha taslimu kwani tunaamini baadhi ya wateja wetu wana ndoto nyingi sana za mafanikio ila tatizo huwa ni pesa ili kitimiza ndoto zao.

Lengo la kampuni yetu ni kuendeleza umoja na mshikamano  na wateja wetu kwa kuutambua na kuuthamini mchango wa wateja wetu kwani wao ni muhimili mkubwa katika kukuza na kuendeleza bai yetu ya Serengeti. Na sasa kampuni ya Serengeti inachezesha promosheni hii kutimiza azma yake ya kuinua uchumi wa wateja wao kama sehemu ya shukrani kwa wateja wake.
Ni wakati wako ndugu mteja kushiriki mara nyingi uwezavyo na kuhakikisha unajishindia zaidi ya milioni saba. Ili kushiriki unatakiwa kufungua chini ya kizibo cha bia ya Serengeti na utakuta namba maalumu na unatakiwa kuituma kwenda namba 15317 na utapokea majibu.
Tafadhari kunywa kistaarabu na ni maalum kwa 18+

Post a Comment

Previous Post Next Post