Lugha ya Kiswahili yazidi kupaa nchini Japani.

IMG_4402

Mke wa Rais na Mwenyekiti  wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Profesa Midori Uno, anayefundisha somo la kiswahili kwenye Chuo Kikuu cha Soka kilichoko huko Tokyo nchini Japan. Mama Salma alikutana na mgeni wake huyo kwenye hoteli ya Intercontinental huko Yokohama leo. PICHA NA JOHN  LUKUWI.
IMG_4493

Na Anna Nkinda – Yokohama
Watumiaji wa  lugha ya Kiswahili wamezidi kuongezeka nchini Japani hadi kufikia hatua ya kuwa na mshindano kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Soka kilichopo nchini humo.
 Hayo yamesemwa leo na Prof.  wa chuo hicho Midori Uno wakati akiongea na Mke wa Rais mama Salma Kikwete alipokutana naye katika hoteli ya Intercontinental mjini Yokohama.
Prof. Uno ambaye ni Mwalimu wa kiswahili katika chuo hicho  alisema kuwa hivi Sasa wananchi wengi  wa Japani wanakiu ya kujifunza na kuzungumza  lugha ya Kiswahili  kwani ni rahisi kueleweka.
“Katika jitihada zangu  za kuwafanya wajapani wengi wajue lugha ya Kiswahili nimetengeneza  kamusi  ya maneno ya kijapani kuwa ya  Kiswahili ambayo watu wengi wanaitumia kwa sasa kwani wengi wajapani wengi wanapenda  kujifunza lugha hii”, alisema Prof. Uno.
Mashindano hayo ya lugha ya Kiswahili ambayo hufanyika mwezi wa kumi na moja kila mwaka huwa ni ya kuandika na kusoma hotuba ambapo mshindi wa kwanza anapewa  cheti, tuzo ya muanzilishi wa chuo hicho, vikombe na zawadi mbalimbali.
Kwa upande wake Mke wa Rais mama Kikwete alimpongeza profesa huyo kwa jitihada zake za kukuza lugha ya  Kiswahili nchini humo na kumuomba aendelee zaidi kufanya hivyo.
Alisema kuwa watanzania wanavitu vyao vya kujivunia kama Taifa,  moja ya vitu hivyo ni lugha ya Kiswahili ambayo imewaunganisha  watanzania wote na kuwa kitu kimoja ndani na n je ya nchi.
Mama Kikwete alisema, “Ili kumfikia mtu mmoja au watu wengi zaidi  ni lazima kuwe  na lugha ya mawasiliano hivyo basi nasi tunatumia lugha hii ambayo iliwaunganisha watanzania wote wakaweza kupigania uhuru wa n chi yao kipindi cha mkoloni”.
Alisema kuwa lugha ya Kiswahili inaongelewa maeneo mengi ya Afrika ya mashariki na ndani ya bara la Afrika na hivi sasa viongozi wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU) waliikubali lugha hiyo kuwa lugha ya mawasiliano .
Profesa Uno alikuja nchini kabla ya kupata uhuru kwa ajili ya kufanya kazi za kujitolea na aliporudi nchini kwake aliamua kuwafundisha wajapani lugha ya Kiswahili pia nchini humo  redio Japani (NHK) inatangaza   matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili ambayo ilianzishwa mwaka 1964

Post a Comment

أحدث أقدم