Machali (Mb) ashambuliwa jana usiku

Picture
 
Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, David Misime amethibitisha taarifa za kuvamiwa na kupigwa kwa mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Joseph Machali (NCCR-Mageuzi).

Kamanda Misime amesema jeshi la polisi mkoni humo linawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo.

Amesema Machali alivamiwa na watu wanne jana usiku alipokuwa akirejea kutoka kwenye vikao vya Bunge.

Kwa sasa Machali amelazwa kwenye hospitali ya mkoa ya Dodoma (General) kwa matibabu zaidi.

Awali, taarifa zilipasha kuwa Machalli akiendesha gari lake meta kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi, aliwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita.

Kitendo hicho  kilionekana kuuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga kwa nguvu bodi ya gari la Machalli jambo ambalo lilimsababish Machalli kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni.

Baada ya kushuka,  vijana hao walimtolea  matusi kadhaa ya nguoni na pindi Machalli aliwajibu kwa hasira ndipo aliposhambuliwa na kupigwa

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia amesema amemkagua Mhe. Machali asubuhi ya leo akia hospitalini na kumkuta anaendelea vyema na matibabu

Post a Comment

Previous Post Next Post