MAJAMBAZI WAVAMIA OFISI YA FILAMU, WAIBA KILA KITU

Bosi wa kampuni hiyo, Alpha Nondo ameliambia Risasi Jumamosi kuwa, majambazi hao waliiba kamera ya kushutia filamu, kinasa sauti ‘bum’, kompyuta na vifaa vingine ambavyo hutumika kurekodia sinema.


MKASA umetokea kwenye Kampuni ya Eagles Entertainment Video inayofanya kazi ya kusambaza filamu, usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, majambazi walivamia ofisi hiyo iliyopo Tabata Kimanga, Dar na kuvunja mlango kisha kuiba vifaa mbalimbali.
 
“Wamevunja mlango na kuiba kila kitu ambacho hutumika kushutia filamu, bahati nzuri tuna vifaa vingine havikuwa ofisini, nadhani walipanga kuiba maboksi ya filamu ya Street Girls si ndiyo ipo sokoni, wakajua mali ipo mle. Lakini tuliripoti Polisi Buguruni,” alisema Alpha.

Post a Comment

أحدث أقدم