Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu na muziki wa Kibongo, Snura Mushi amefikia uamuzi wa kuachana na mpenzi wake anayejulikana kwa jina moja la Ommy Crazy ambaye ni DJ wa Maisha Club ya jijini Dar.
Snura Mushi.
Baada ya kuzinyaka habari hizi paparazi wetu alimtafuta Snura ili kusikia kauli yake ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli nimeachana na Ommy kwa kuhofia majanga ya mapenzi maana nimegundua kuwa siyo mkweli kwenye uhusiano wetu.”
Staa huyo ambaye hivi sasa anatamba na ngoma yake ya Majanga aliongeza kuwa ameona ni heri akomae na muziki kuliko kuendekeza wanaume.
“Unajua miye nikikosewa na mwanaume huwa nachanganyikiwa kiasi cha kushindwa hata kufanya shoo, hivyo nimeona ili nisiharibu muziki wangu ni heri tuachane na Ommy,” alisema Snura.
Aidha, aliongeza kuwa nafasi aliyokuwa nayo sasa katika muziki ameisotea kwa muda mrefu, hivyo anapaswa kuilinda kwa nguvu zake zote ili aendelee kung’ara.
إرسال تعليق