Ndugu zanguni,
Kwanza kabisa nawapa pole ndugu zetu wa Arusha kwa tukio la kusikitisha lililotokea kwenye mkutano wa Chadema. Ppia nawapa pole wafiwa na nawaombea waliojeruhiwa wapone haraka.
Nimegudua kuwa sasa hapa jamvini wanachama wa CCM na Chadema wanatupiana lawama kuhusu tukio la leo na kila mmoja anamnyooshea kidole mwenzake kuwa amehusika kwa njia moja ama nyingine
Lakini ningependa kuwakumbusha jambo moja tu.
Inawezekana kabisa kuwa kuna mtu au kikundi cha watu fulani kimeamua kufanya mauaji yake kwa kutumia kivuli cha siasa. Inawezekana kabisa kuwa wanafanya haya mauaji wakijua kuwa yakitokea mara moja tutaanza kunyoosheana vidole wenyewe na wao wanakaa pembeni wanatucheka.
Nawaomba tu niwakumbushe kuwa kuna padre alipigwa risasi kule zanzibar na siku chache baadae bomu likalipuka kanisani na leo kwenye mkutano.
Tunasahau yote na matokeo yake tunanyoosheana vidole. Mimi ningeomba tu wakati tunanyoosheana vidole tuangalie na uwezekano wa watu wenye nia mbaya ya kutuvurugia amani kutumia mwanya huu kwa kuendeleza mauaji. Ni sawa tu na mtu amfinye makalio mtu alie mbele yako halafu ajikaushe, moja kwa moja aliefinywa atadhani ni wewe ulie nyuma yako na nyote mtaanza kudundana huku jamaa anawacheka.
Lakini pia tusisahau jinsi Ludo alivyojiteka ili aonekane victim wakati yeye ndio mshitakiwa nambari moja.
Wengine wako tayari nchi isitawalike na watu wauawe ili waingie ikulu
Nawaomba wale wote wenye kujua lolote watoe taarifa polisi na pia nawaomba polisi wajenge utaratibu wa kutoa donge nono kwa wanachi waoawasaidia kwenye uchunguzi ili kujenga morale ya kuisaida polisi
MUNGU IBARIKI TANZANIA
إرسال تعليق