Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athmani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea juzi hivi karibuni katika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.
JESHI la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Masomo ya Ziada akituhumiwa kumbaka Mwanafunzi wa darasa la nne mwenye umri wa miaka 10.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea hivi karibuni katika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Ipyana Gidion (30) mkulima na mwalimu wa masomo ya ziada (tuition) katika kituo cha Itunge Moravian mtaa wa Mbugani Wilayani Kyela Mkoani hapa.
Alisema Mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto mwenye umri wa miaka 10, kyusa,mwanafunzi darasa la nne katika Shule ya msingi Mbugani mkazi wa Itunge “a” na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Kamanda Diwani alisema mbinu iliyotumika ni kuwaruhusu wanafunzi aliokuwa akiwafundisha kuondoka na kubaki na mhanga kisha kumbaka katika chumba anachotumia kufundishia (darasani).
Aliongeza kuwa mtuhumiwa aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka na kutoka kwa rufaa na kwamba mhanga amepatiwa matibabu na kuruhusiwa ambapo taratibu zinafanywa ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani
MBEYA YETU
|
Post a Comment