Mkuu
wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi akiwa amempakatia mtoto wa
kiume ambaye inadaiwa kutelekezwa kwenye pagara la nyumba na mama yake
ambaye anasoma chuo cha uhasibu tawi la Singida.Mtoto huyo mwenye umri
wa miezi mitano, amehifadhiwa wodi sita (b) katika hospitali ya mkoa
mjini Singida.
Na Nathaniel Limu.
Mwanafunzi
wa kike wa chuo cha uhasibu tawi la mkoa wa Singida ambaye hajafahamika
jina lake, amemtelekeza mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miezi mitano
ndani ya jengo la nyumba (pagala) ambayo bado haijamalizika kujengwa.
Mkuu
wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, amesema mwanafunzi huyo
ametenda unyama huo usiku katika kijiji cha Misake nje kidogo ya Singida
mjini.
Amesema motto huyo mwenye afya njema kabisa, ameokotwa na raia wema baada ya kusikia akilia ndani ya pagala la nyumba.
Mlozi amesema kwa mujibu wa raia hao wema, walikuta mtoto huyo akiwa ametandikiwa shuka vizuri na kufunikwa kwa blakenti ndogo.
Mkuu
huyo wa wilaya amesema jeshi la polisi limechukua kadi ya kliniki
iliyotolewa na zahanati ya Mandewa ili kufuatilia jina la mama na baba
wa mtoto huyo.
Amesema
taarifa zilizopatikana eneo la tukio, zanadai kuwepo kwa mwanafunzi wa
uhasibu aliyekuwa akiishi na mtoto kwenye hosteli na baada ya tukio
mwanafunzi huyo ametoweka.
إرسال تعليق