Nchini Uganda - Wafanyabiashara wagoma

Maduka yamesalia kufungwa mjini Kampala Ugana kwa siku ya tatu leo huku wafnyabiashara wakigoma kuhusiana na mpango wa serikali kusisitiza viwango vya biadhaa zinazoingizwa nchini humo kuwa za juu.
Chama cha wafanyabiashara hao kinasema kinapinga gharama wanayotozwa ikiwa bidhaa wanazoingiza nchini humo sio za viwango vya juu. Malipo hayo ni kodi iliyoanza kutozwa na serikali hivi karibuni ambayo inagharamia kuchunguzwa kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo
Wanatak serikali ikome kuwatoza ushuru huo kwani wafnyabiashara tayari wanatozwa kodi ya juu.
Duru zinasema kuwa vuguvugu la upinzani linatarajiwa kujiunga na maandamano hayo, na kuwa polisi wamedhibiti hali ya usalama mjini Kampala.
Mwandishi wa BBC mjini humo Catherine Byaruhanga anasema kuwa polisi huenda wakavunja maandamano hayo kwa kuhofia otovu wa usalama.
Waziri wa biashara, Amelia Kyambadde, ameelezea wazi kuwa Uganda inashinikizwa na wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa iweze kutekeleza vikwazo vya kuhakikisha kuwa bidhaa zinzoingizwa nchini humo ziwe za hali ya juu.
Kodi hiyo inalenga kuondoa uwezekano wa wafanyabiashara kuingiza biadhaa ghushi nchi humo swala ambalo Uganda inatuhumiwa kutokuwa maakini nalo katika kulitokomeza.
Wafanyabiashara wanapaswa kuingiza nchini humo bidhaa za hali ya juu kutoka kwa watengezaji wanaojulikana na ambao wako kwenye orodha inayojulikana kwa mataifa ya Afrika Mashariki, ingawa wanasema kuwa gharama inayopaswa kulipwa kwa hilo kufanyika ni ya juu zaidi.

Post a Comment

أحدث أقدم