New track:- Stara Thomas na Linex Isikilize Hapa

Tunafahamu Stara Thomas staa wa longtime kwenye bongofleva amerudi kuendelea kufanya muziki wa bongofleva baada ya kutangaza kuuacha wakati alipoamua kuokoka na kumpokea Yesu lakini imebidi arudi na kutangaza msimamo wake wa sasa kwamba ili aweze kuendesha maisha yake kiuchumi ni lazima afanye bongofleva. Hii haimaanishi kwamba anaachana na Gospel bali atakua anafanya gospel na bongofleva kwa wakati mmoja huku akiwa bado kaokoka akiamini bongofleva sio uhuni…….. ni kazi kama kazi nyingine. Baada ya hizo sentensi hapo juu naomba upokee mwaliko wa kuisikiliza single yake mpya hapa chini…

Post a Comment

Previous Post Next Post