Polisi Afukuzwa Kazi kwa Kupiga picha za Uchi Magomeni


POLISI wa kike wa Kituo cha Magomeni, jijini Dar es Salaam aliyejulikana kwa jina moja la Anisa, ametimuliwa kazi  kwa madai ya kupiga picha ya utupu iliyosambaa mitandaoni.
Chanzo makini ndani ya jeshi hilo kilisema Anisa alifukuzwa kazi wiki iliyopita baada ya kuhojiwa na mabosi wake wa makao makuu ya jeshi hilo na kukiri kuwa picha hiyo ni yake.
“Anisa aliitwa makao makuu, mabosi wakamuonesha picha yake akiwa mtupu kitandani, akakiri ni yeye. Alijitetea eti alifanya hivyo kwa sababu siku ya tukio alikuwa amelewa sana,” kilisema chanzo.
Chanzo kiliendelea kudai kwamba baada ya afande huyo mwenyeji wa Tanga kukiri, viongozi wa jeshi hilo walimwambia amekiuka kanuni na kulidhalilisha jeshi hilo hivyo hataendelea kuwa mtumishi.
Picha ya afande huyo imeenea mitandaoni na kwenye baadhi ya simu za mikononi za watu kitendo kulicholifanya jeshi hilo kufanya uchunguzi na kubaini kuwa ni yake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina, Suleiman Kova alipoulizwa  juzi alikiri kufukuzwa kwa askari huyo na kumtaka mwandishi wetu kufuatilia zaidi kwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura ambaye naye alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikiri.
‘‘Tunahitaji askari wenye maadili mema ndani ya jeshi letu, yule atakayefanya mambo bila kufuata kanuni na sheria hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Askari muda wote anatakiwa awe mfano bora kwa  jamii,’’ alisema Afande Wambura.
Taarifa zaidi zinadai kwamba kwa sasa Anisa anaishi uraiani kama raia wa kawaida

Post a Comment

أحدث أقدم