PPF YAONGEZA MUDA WA KUSOMESHA WATOTO MPAKA KIDATO CHA SITA



Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele akielezea kuhusu miaka 35 tangu kuanzishwa kwa PPF mwaka 1978 wakati wa mkutano na wanahabari leo katika Ofisi za PPF Makao Makuu. Mkutano huo ulielezea mafanikio Mbali mbali ya Mfuko pamoja na PPF kuoongeza muda wa kuwasomesha watoto wa wanachama kutoka kidato cha nne mpaka cha sita. Vilevile katika kusheherekea miaka 35 PPF itakuwa na wiki ya huduma kwa wateja kuanzia tarehe 1 Julai mpaka tarehe 5 Julai 2013 ambapo wanachama wanaombwa kufika kwa wingi kwenye ofisi za Mkoa wa Dar es salaam ili kuweza kuendelea kujua shughuli mbalimbali zitolewazo na Mfuko wiki, hiyo itaenda sambamba na maonyesho ya sabasaba ambapo Mfuko wa PPF utakuwa na banda katika viwanja vivyo. Sherehe za miaka 35 zitafikia kilele katika Mkutano wa 23 wa wanachama na wadau utakaofanyika mwezi wa 10 mwaka huu.Kushoto ni Meneja Huduma kwa Wanachama Bw. Godfrey Mollel

Post a Comment

أحدث أقدم