QUICK ROCKA KUTOKA NA “MY BABY” TAREHE 21, KAA TAYARI KUPOKEA MZIGO HUO


Quick Rocka ambae siku za nyuma kidogo alitupa kionjo cha ngoma na video yake mpya ambayo ameshirikiana na marehemu Mangwea na mwanadada Shaa inayokwenda kwa jina la My BABYambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni …
Sasa baada ya kionjo hicho, Quick anatarajia kuachia ngoma hiyo tarehe 21 mwezi huu katika ukumbi wa disco wa Ambassadors Lounge uliopo mjini Dar es Salaam katika jengo la Benjamin Mkapa Tower
Katika uzinduzi wa ngoma hiyo ambayo itakuwa na video pia, Quick atasindikizwa na baadhi ya wasanii ambao ni pamoja na Mirror, Stamina, Izzo Bizness pamoja na Young Killer …

Post a Comment

Previous Post Next Post