Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesafiri hii leo kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini Uganda. Hii ni ziara ya kwanza ya rais huyo katika nchi jirani ya Uganda tangu kuchukua uongozi wa taifa hilo katika uchaguzi uliofanyika miezi mitatu iliyopita.
Rais Kenyatta anafanya ziara hii kwa mwaliko wa rais Yoweri Museveni ambaye alikuwa Kiongozi wa pekee wa taifa ya nje aliyetoa hotuba katika sherehe ya kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta, ambapo alikemea mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC kwa kuwalenga viongozi wa Afrika katika oparesheni zake.
Rais Kenyatta na naibu wake wamefunguliwa mashtaka katika mahakama hiyo ya ICC ya kuhusika na machafuko ya baada ya uchaguzi nchini humo mwaka wa 2008.
Rais Museveni ni mmoja wa vingozi wa Afrika wanaopinga mahakama ya ICC akisema kuwa inalenga kuwadhulumu waafrika kauli iliyotolewa na viongozi wa Afrika walipokutana kwenye mkutano wa mataifa ya Afrika au AU mjini Addis Ababa Ethiopia ambpo waliikemea sana mahakama hiyo.
Kwa sasa haijulikani ikiwa swala la ICC litakuwa kwenye ajenda ya mkutanao wa viongozi hao.
إرسال تعليق