Wananchi wa Brazil wakiwa katika maandamano yaliyoambatana na vurugu nchi nzima wakidai huduma bora za Umma.
Rais wa Brazil Dilma Roussef ameitisha mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri hii leo ikiwa ni siku moja baada ya muandamanaji mmoja kuuawa na wengine takriban milioni 1.25 wakifanya maandamano kote nchini wakidai huduma bora za umma.
Maandamano hayo makubwa ambayo baadhi ya wakati yamekuwa yakigeuka vurugu yanafanyika wakati nchi hiyo ikizikaribisha timu kadhaa kutoka kote ulimwenguni katika mashindano ya soka ya kuwania kombe la mabara-Confederation Cup-, ikiwa ni michuano ya kuelekea kombe la dunia nchini humo mwaka ujao.
Katika mji wa Rio,polisi wa kukabiliana na fujo walifyatua gesi za kutowa machozi na risasi za mpira dhidi ya waandamanaji.Waandamanaji hao wanapinga rushwa na huduma mbaya katika sekta za umma
Post a Comment