Demonstrators hoild a protest in Rio de Janeiro, one of many such protests in Brazil's major cities, June 20, 2013. Tens of thousands of demonstrators marched through the streets of Brazil's biggest cities on Thursday in a growing protest that is tapping into widespread anger at poor public services, police violence and government corruption. The signs reads, "Wake up Brazil", "As the football rolls, we're missing health and schools", and "Hospital of FIFA standard." REUTERS/Luciana Whitaker (BRAZIL - Tags: CIVIL UNREST POLITICS)
 Wananchi wa Brazil wakiwa katika maandamano yaliyoambatana na vurugu nchi nzima wakidai huduma bora za Umma.
Rais wa Brazil Dilma Roussef ameitisha mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri hii leo ikiwa ni siku moja baada ya muandamanaji mmoja kuuawa na wengine takriban milioni 1.25 wakifanya maandamano kote nchini wakidai huduma bora za umma.
Maandamano hayo makubwa ambayo baadhi ya wakati yamekuwa yakigeuka vurugu yanafanyika wakati nchi hiyo ikizikaribisha timu kadhaa kutoka kote ulimwenguni katika mashindano ya soka ya kuwania kombe la mabara-Confederation Cup-, ikiwa ni michuano ya kuelekea kombe la dunia nchini humo mwaka ujao.
Katika mji wa Rio,polisi wa kukabiliana na fujo  walifyatua gesi za kutowa machozi na risasi za mpira dhidi ya waandamanaji.Waandamanaji hao wanapinga rushwa na huduma mbaya katika sekta za umma