alupo-20130319-231201
 Waziri wa Elimu nchini Uganda Jessica Alupo.
 Shule kadhaa za Sekondari za binafsi nchini Uganda zimepinga tathmini iliyotolewa na Na Wizara ya Elimu nchini humo.
Takwimu hizo zinahusisha shule za Gulu Central High School, St. Mary’s College Lya ugazi na St. Mary’s Kitende kuwa ndio bora.
Tathmini hiyo inayohusisha afya na usalama sambamba na uwepo wa waalimu bora, ustawi na maendeleo imezipa kiwango cha 828 kati ya zaidi ya shule 4,000 za binafsi zilizopo nchini Uganda.
Kwa kuangalia ubora na uhitimu wa wanafunzi shule ya St. Mary’s ya Kitende na mara kwa mara imekuwa ikipewa kiwango kikubwa wakati nyingine zimeachwa .
 George William Ndugwa wa Shule ya Baptist High ya Kitebi amesema shule hiyo haikutambelewa wala kukaguliwa wakati wa kuandaa ripoti ya hivi karibuni na pia taarifa iliyopita haikufanywa kwa uangalifu kuhusu shule hiyo.
Taarifa hiyo imehusisha utawala boara wa shule, miundo mbinu na mfumo mzima wa shule na uendelevu wa kifedha pia shughuli nzima za kimtaala kwa wanafunzi.
Hii inakuwa mara ya pili Afroeducare inatoa viwango kwa shule nchini humo japo shule kadhaa hazikukaguliwa kufuatia wakurugenzi wa shule hizo kupinga mbinu zinazotumika huku shule nyingine zikionyesha ushirikiano