Mabingwa Manchester United. |
Ratiba ya Ligi Kuu soka nchini Uingereza imetoka leo(Juni 19,2013) na mechi ya kwanza ya David Moyes nyumbani kama kocha mpya wa Manchester United itakuwa dhidi ya Cheslea yenye kocha mpya pia, Kocha Jose Mourinho.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu, Manchester United watakuwa na mwanzo mgumu katika ligi hiyo msimu ujao 2013-14 wakisafiri kuwafuata Liverpool na Manchester City ndani ya mechi tano za mwanzoni.
Mechi ya kwanza kwa Meneja mpya wa Manchester City,Kocha Manuel Pellegrini, ni Nyumbani Uwanja wa Etihad kwa kucheza na Newcastle.
Kocha David Moye. |
Manchester United itaanza na mabingwa wa Kombe la Ligi, Swansea Agosti 17, kabla ya kurejea nyumbani kumenyana na Mourinho na Chelsea yake Old Trafford wikiendi inayofuata.
Mechi na Liverpool itafuatia Agosti 31 kabla Dabi ya kwanza ya Jiji la Manchester itachezwa hapo Septemba 21 Uwanja wa Etihad kati Manchester City na Manchester United na Marudiano ni Old Trafford Machi 1.
Arsenal wataanza Msimu wao wakiwa Nyumbani Emirates kwa kucheza na Aston Villa huku Liverpool pia wakiwa Nyumbani kuivaa Stoke City na Tottenham wataanza Ugenini dhidi ya Timu iliyopanda Daraja Crystal Palace.
Zilizopanda:Hull (Picha Juu ) na Cardiff (picha chini) zote zitacheza nyumbani mechi za kufunga msimu wa Ligi kuu Uingereza 2013/2014.
|
MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU ENGLAND 2013/2014 ni (AGOSTI 17,2013).
Arsenal v Aston Villa
Chelsea v Hull City
Crystal Palace v Tottenham Hotspur
Liverpool v Stoke City
Manchester City v Newcastle United
Norwich City v Everton
Sunderland v Fulham
Swansea City v Manchester United
West Bromwich Albion v Southampton
West Ham United v Cardiff City
إرسال تعليق