Kikosi cha Ruvu Shooting
KLABU ya soka ya Ruvu
Shooting imeizidi kete klabu ya Simba kwa kumsajili mchezaji wa Azam
Fc Cosmas Ader aliyekuwa akiicheza kwa mkopo katika klabu ya African Lyon.
Ader ni mshambuaji chipikizi
mwenye kipaji cha hali ya juu alikuwa akiwania pia na klabu ya Simba kabla ya
juzi kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Ruvu Shooting.
Ofisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire alisema usajili wa mchezaji huo ndio
mwanzo wa harakati za kukiimarisha kikosi chao lwa ajili ya msimu ujao wa ligi
kuu soka Tanzania Bara.
Alisema katika kukiimarisha
kikosi chao wanatarajiwa kusajili wachezaji watano wapya na kwamba wanafanya
usajili wao kimya kimya ili kuepuka kuchezewa rafu zisizo na maana ambazo
zimezoeleka katika usajili wa wachezaji hapa nchini.
“Tunapenda kuutangazia umma
wa wapenda soka kwamba Ader kuanzia sasa ni mali ya Ruvu Shooting hivyo klabu
yoyote isijusumbue kufanya naye mazungumzo,”alisema
Ader mwenye kipaji cha aina
yake alikuwa ni mmoja ya wachezaji waliowezesha timu ya Vijana ya Azam kutwaa
ubingwa wa kombe la Uhai kwa miaka miwili mfululizo 2009 na 2010.
إرسال تعليق