Tamasha la Tigo Mini Kabaang kufanyika jijini Mwanza Jumapili hii.


DSC_0599


DSC_0608

Msanii wa bongo flava Diamond Platnumz akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya Jumapili pembeni yake meneja chapa ya TigoTanzania Bw. William Mpinga.
DSC_0618
Msanii Madee akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake meneja chapa ya TigoTanzania bw.William Mpinga na Diamond Platinumz.
DSC_0623
Msanii Richie Mavoko akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika  mjini Mwanza siku ya Jumapili kulia kwake ni Msanii Madee, meneja wa Tigo Bw. William Mpinga na Diamond Platniumz.
Msanii Bora wa mwaka Diamond Platinumz, Fid Q na wasanii wengine sita wanatarijiwa kupagawisha mashabiki zaidi ya elfu sitini katika tamasha la Tigo Mini Kabaang litakayofanyika jijini Mwanza (Rock city) Jumapili hii ya Juni 30.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo, Meneja wa Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga alisema kwamba lengo la tamasha hilo ni kujenga mahusiano ya karibu na wateja wao kwa  kutumia sanaa ya muziki kama njia ya kutangaza huduma za Tigo na bidhaa zake za vifurushi kwa wateja wengi zaidi.
“Tunaamini kwamba tamasha hili litajenga mazingira mazuri yakufanya kampuni na wateja wetu kuelewana zaidi.  Mwisho wa siku tunatarajia wateja wetu kujumuika nasi, kupata burudani yakutosha na kuelimishwa zaidi kuhusu huduma zetu mbali mbali zenye ubora na unafuu kama Mini Kabaang,” alisema Mpinga.
Mini Kabaang inatoa muda wa maongezi wa dakika 20 za bure, 50MB ya kifurushi cha intaneti, pamoja na ujumbe mfupi 100 kwa shilingi 475 tu kwa siku.
Mkutano huo wa waandishi wa habari pia ulihudhuriwa na wasanii wakubwa kama Madee wa Tip Top, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Richi Mavoko, Recho, Kazi Kwanza, Diamond Platnumz na Fid Q, ambao ndio wasanii wa Bongo Fleva watakaopamba siku hiyo ya Jumapili katika viwanja vya CCM Kirumba kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.
“Mimi pamoja na wasanii wenzangu tunayo furaha kubwa kushiriki katika tamasha la Tigo Mini Kabaang litakalofanyika jijini Mwanza, hakika watu wa Rock city ni washabiki wakubwa wa muziki wetu, na tunatarajia kwenda kuwapa burudani ya kutosha,” alieleza Diamond Platnumz alipoulizwa kuhusu tamasha hilo.
“Binafsi nina furaha yakipekee kufanya tamasha langu la kwanza la wazi jijini Mwanza. Naamini hao mashabiki elfu sitini na zaidi wataonyesha  mapenzi ya dhati kwa muziki wangu. Ninahamu sana ya kufika na kufanya tamasha hii,” aliongeza super staa huyo.
“Tamasha hili la Tigo Mwanza Mini Kabaang pia litawapa fursa mashabiki kujishindia zawadi mbali mbali kama vile simu, vocha, fulana za nembo ya Tigo na nyingine nyingi. Hakutakuwa na kiingilio siku hiyo, tunapenda kuwakaribisha kila mteja wa Tigo na mshabiki wa bongo fleva kujumuika na kushiriki nasi,” aliongezea Mpinga.
“MINI KABAANG” ni kifurushi cha siku ambacho mteja akijiunga anapata dakika 20 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao wowote ule, pia anapata kifurushi cha 50MB ya intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi 100 kwa mtandao wowote. Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi apige namba *148*01#. Huduma hii inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kwa gharama nafuu ya shilingi 475 tu kwa siku.
Tamasha za Mini Kabaang ni mfululizo wa maonyesho ya muziki yanayoandaliwa na Tigo, yamekwisha fanyika Morogoro, Moshi na sasa Mwanza. Mikoa mengine itakayofuata ni Mbeya, Dodoma na mikoa mingine.

Post a Comment

Previous Post Next Post