Msanii
wa bongo flava Diamond Platnumz akizungumza na waandishi
wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang
litalofanyika mjini Mwanza siku ya Jumapili pembeni yake meneja chapa ya
TigoTanzania Bw. William Mpinga.
Msanii
Madee akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha
kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili
pembeni yake meneja chapa ya TigoTanzania bw.William Mpinga na Diamond
Platinumz.
Msanii
Richie Mavoko akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu
tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya Jumapili kulia kwake ni Msanii Madee, meneja wa Tigo Bw. William Mpinga na Diamond Platniumz.
Msanii
Bora wa mwaka Diamond Platinumz, Fid Q na wasanii wengine sita
wanatarijiwa kupagawisha mashabiki zaidi ya elfu sitini katika tamasha
la Tigo Mini Kabaang litakayofanyika jijini Mwanza (Rock city) Jumapili
hii ya Juni 30.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo, Meneja wa Chapa wa Tigo Bw.
William Mpinga alisema kwamba lengo la tamasha hilo ni kujenga
mahusiano ya karibu na wateja wao kwa kutumia sanaa ya muziki kama njia
ya kutangaza huduma za Tigo na bidhaa zake za vifurushi kwa wateja
wengi zaidi.
“Tunaamini
kwamba tamasha hili litajenga mazingira mazuri yakufanya kampuni na
wateja wetu kuelewana zaidi. Mwisho wa siku tunatarajia wateja wetu
kujumuika nasi, kupata burudani yakutosha na kuelimishwa zaidi kuhusu
huduma zetu mbali mbali zenye ubora na unafuu kama Mini Kabaang,”
alisema Mpinga.
Mini
Kabaang inatoa muda wa maongezi wa dakika 20 za bure, 50MB ya kifurushi
cha intaneti, pamoja na ujumbe mfupi 100 kwa shilingi 475 tu kwa siku.
Mkutano
huo wa waandishi wa habari pia ulihudhuriwa na wasanii wakubwa kama
Madee wa Tip Top, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Richi Mavoko, Recho,
Kazi Kwanza, Diamond Platnumz na Fid Q, ambao ndio wasanii wa Bongo
Fleva watakaopamba siku hiyo ya Jumapili katika viwanja vya CCM Kirumba
kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.
“Mimi
pamoja na wasanii wenzangu tunayo furaha kubwa kushiriki katika tamasha
la Tigo Mini Kabaang litakalofanyika jijini Mwanza, hakika watu wa Rock
city ni washabiki wakubwa wa muziki wetu, na tunatarajia kwenda kuwapa
burudani ya kutosha,” alieleza Diamond Platnumz alipoulizwa kuhusu
tamasha hilo.
“Binafsi
nina furaha yakipekee kufanya tamasha langu la kwanza la wazi jijini
Mwanza. Naamini hao mashabiki elfu sitini na zaidi wataonyesha mapenzi
ya dhati kwa muziki wangu. Ninahamu sana ya kufika na kufanya tamasha
hii,” aliongeza super staa huyo.
“Tamasha
hili la Tigo Mwanza Mini Kabaang pia litawapa fursa mashabiki
kujishindia zawadi mbali mbali kama vile simu, vocha, fulana za nembo ya
Tigo na nyingine nyingi. Hakutakuwa na kiingilio siku hiyo, tunapenda
kuwakaribisha kila mteja wa Tigo na mshabiki wa bongo fleva kujumuika na
kushiriki nasi,” aliongezea Mpinga.
“MINI
KABAANG” ni kifurushi cha siku ambacho mteja akijiunga anapata dakika
20 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda
mtandao wowote ule, pia anapata kifurushi cha 50MB ya intaneti na kuweza
kutuma ujumbe mfupi 100 kwa mtandao wowote. Kutumia kifurushi hiki
mteja anabidi apige namba *148*01#. Huduma hii inapatikana kwa wateja
wote wa Tigo kwa gharama nafuu ya shilingi 475 tu kwa siku.
Tamasha
za Mini Kabaang ni mfululizo wa maonyesho ya muziki yanayoandaliwa na
Tigo, yamekwisha fanyika Morogoro, Moshi na sasa Mwanza. Mikoa mengine
itakayofuata ni Mbeya, Dodoma na mikoa mingine.
إرسال تعليق