1] Aston Villa wanajipanga na uhamisho wa Darren Bent na wanataka pauni milioni 8, hii ni hasara kwa Villa sababu walimnunua Bent kwa gharama mara tatu ya bei wanayo muuza. Bent ametulia na Villa toka Januari 2011. Club ya New Castle ndio iko mstari wa mbele kumnasa Bent.
Darren Bent Amefunga Magoli 21 ndani ya mechi 54 za Premier League akichezea Villa. Kwa sasa Bent analipwa vizuri sana pale Villa, kumtoa inakuwa ngumu unless club iko tayari kumpa mshahara mzuri, anachukua pauni milioni 3 kwa mwaka.
2] Liverpool wako mbioni kukamilisha uhamisho wa Christian Atsu kutoka Ghana.Jamaa kwa sasa yuko Porto na wanataka pauni milioni 3.
Atsu ni winger mwenye miaka 21 amesema hataki mkataba mwingine na Porto.
3]Inasemekana Liverpool wako na dili nyingine ya kukamilisha ndani ya saa 48, inamuhusu Luis Alberto kutoka Seville kwa gharama ya pauni milioni 6. Uhamisho huu unategemewa kukamilika mapema wiki hii na mchezaji huyu atakuwa Uingereza mwisho wa wiki. Kwa sasa anaichezea Sevilla FC kama mshambuliaji.
Post a Comment