TAARIFA
ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo
Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka
zimevujaKwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi
(jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya
Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa hana ujauzito tena kama wengi
wanavyodhani.
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.
Hata
hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha
kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia
vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi
kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali
alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na
ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lililimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Mwandishi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
Mwandishi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine?
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.
Mwandishi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.
Mwandishi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine?
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.
Source:Talk Bongo Blog
Post a Comment