TIGO YACHANGIA MILIONI 30 KATIKA KAMPENI YA UCHANGIAJI WA DAMU


Afisa Mahusiano ya Jamii na Matukio wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael, akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 30 Mkurugenzi wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Efesper
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiudhuria press conference
Afisa Mahusiano ya Jamii na Matukio wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi msaada wa shilingi milioni 30 kwa Mpango wa Taifa
Kampuni ya Tigo Tanzania, kwa mara nyingine tena leo imehaidi kuunga mkono suala muhimu la maadhimisho ya siku ya  uchangiaji damu kwenye siku ya dunia ya wachangiaji damu yatakayofanyika mkoani Mara tarehe 14 Juni, 2013. Zoezi hili lakuchangia damu yatafanyika katika mikoa yote hapa nchini  yetu ambapo uzinduzi wa mpango hu wa taifa  hutafanyika mkoani mara  kitaifa zitafanyika mkoani Mara nakuendelea katika mikoa mengine hapa nchini.  
“Huduma ya kuchangia damu kwa mara nyingine imevutia kufanyiwa kazi na Tigo katika juhudi za kuinua uelewa wa jamii juu ya umuhimu wa kujitolea kuchangia damu katika kuhakikisha upatikanaji wa damu salama na ya kutosha. Zoezi hili la uchangiaji wa damu litarajia kupunguza, kwa kiasi kikubwa, uhaba wa damu uliopo hivi sasa unaozikabili hospitali nyingi nchini, na kwa maana hiyo kuwezesha kuzuia vifo visivyo vya lazima, hususa, kwa wanawake na watoto ambao ndio wahitaji wakuu wa damu…. Ningependa kuchukua fursa hii kuishukuru kampuni ya Tigo kwa msaada wake imara kwenye mpango huu unaolenga kuwapatia Watanzania maisha bora na yenye afya”. Alisema Dk. Efesper A. Nkya, program meneja wa mpango wa NBTS
Afisa Mahusiano ya Jamii na Matukio wa Kampuni ya  simu za mkononi ya Tigo , Woinde Shisael  alisema; “Kampuni ya Tigo inajisikia fahari  kwa  kuwemo kwake katika mpango huu wenye lengo la kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa uchangiaji damu salama, huku tukiwashukuru wachangiaji damu waliopo na pia kutoa wito kwa wachangiaji wapya kujitokeza kuchangia damu. Afya ya jamii ni muhimu sana kwa kampuni ya Tigo na hivyo kuifanya Tigo kujihususha kikamilifu katika mpango huu. Hili ni jambo linalohitaji msaada wa kila mmoja wetu”.
Shisael  aliongeza kusema kwamba; “ Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba Watanzania wote  kuipa muhimu unaostahili suala hili na kujitokeza kuchangia damu na hivyo kuokoa maisha ya wahitaji kama kaulimbiu ya mwaka 2013 inavyosema “Kila mchango wa Damu  ni zawadi kwa maisha”. Tigo itaendelea kushirikiana na kuwekeza katika sekta ya afya nchini  kwajili yakuhakikisha kwamba   Watanzania wote wanaendelea kua na afya nzuri.
Siku ya uchangiaji damu duniani ni mpango uliobuniwa ili kuelimisha kuhusu umuhimu wa damu salama, kuhamasisha uchangiaji damu wa hiyari na pia kuwashukuru wachangiaji damu bila malipo  kwa mchango wao mkubwa katika kuokoa maisha. Kaulimbiu ya kampeni ya dunia ya uchangiaji damu 2013 inasema “Kila mchango wa Damu nikama  zawadi wa maisha kwa binadam”.
Kuhusu  Huduma ya kutoa Damu ya Taifa

NBTS ilianzishwa mwaka 2004 na ni mpango chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii(MoHSWna mamlaka ya kuhakikisha upatikanaji wa damu salama ya kutosha kupitiaserikali kuu ni uratibu wa huduma ya kuongezewa damu nchin Tanzania
Ni ya malengo makuu ni:
1. Kuongeza uwezo wa kukusanya, usindikaji na kusambazaji wa kutosha wa damu salama na damu kutoka kwa wafadhili wa hiari ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa.
2. Ili kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kutosha na kupatikana ya damu salama kutoka kwa  wafadhili  wa  damu  kutokana na idadi ya watu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3. Kuanzisha ufuatiliaji na tathmini ya mfumo wa kudumisha ubora, na ufanisi wa Huduma ya
 Damu ya Taifa.

NBTS inafanya kazi nchi nzima na JWTZ na TRCs kama washirika wake kupitia vituo vyake sita ambavyo ni  Kanda ya Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Mtwara, Mbeya na Moshi.
Kama mdau TACAIDS wamechangia sana katika kuzuia VVU / Ukimwi, tangu kuanzishwa kwake, na kupunguza kwa kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU, na ni miongoni mwa wafadhili damu kutoka% 7-10 mwaka 2004 hadi 1.2% katika 2012.

Post a Comment

أحدث أقدم