Meneja wa data kasi (Broadband) wa mtandao wa Tigo Bw. Benedict Mponzi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu mpya aina ya Ascend Y300. Katikati niMkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Huawei Technologies Tanzania Bw.Zhang Yong Quan.
Tigo Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Huawei Technologies Tanzania leo wamezindua aina mpya ya simu za mkononi zenye ubora wa hali ya juu kabisa na gharama nafuu aina ya ‘Ascend Y300’.
“Simu hizi za Huawei ‘Ascend Y300’ ni nzuri na bora na zilizotengenezwa kwa umahiri mkubwa zinapatikana kwa bei nafuu na tunaamini kuwa zitakuwa ni chaguo la wengi kama ilivyokuwa simu za ‘Ascend Y200. Tunayo furaha kwa mara nyingine tena kushirikiana na Tigo Tanzania na tunaimani kubwa kuwa mahusiano yetu yataendelea kukua na kuimarika zaidi kwenye kutoa suluhisho la huduma mpya na nzuri za mawasiliano Tanzania..” alifafanua Zhang Yong Quan, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Huawei Technologies Tanzania.
Ascend Y300 ni maalumu kabisa katika soko la sasa. Iina kioo chenye ukubwa wa inchi 4, processor yenye uwezo wa 1GHz, na ina seli yenye uwezo mkubwa wa kutunza chaji. Simu zimetengenezwa maalumu kukidhi mahitaji ya watumiaji wa mitandao ya kijamii na matumizi yake ni rahisi kabisa. .” aliendelea kufafanua Bw. Yong Quan.
Meneja wa data kasi (Broadband) wa mtandao wa Tigo Bw. Benedict Mponzi alisema “Tigo inajivunia kwa mara nyingine tena kushirikiana na kampuni ya Huawei Technologies kwa kuwapatia watanzania kile wanachokitaka. Kutokana na ongezeko kubwa la watumiaji wa huduma za intaneti, simu maalumu za ‘smartphones’ zimekuwa ni chombo cha lazima, na simu mpya aina ya ‘Ascend Y300’ ni suluhisho kwa Watanzania wote kwani ina uwezo mkubwa sana wa mawasiliano ya mtandao wa simu na intaneti, tena kwa bei poa!
Ushirikiano madhubuti kati ya Tigo na Huawei ni jitihada maalumu yenye lengo la kuwapatia wateja wetu wapendwa wa Tigo suluhisho la mawasilino ya simu kwa ujumla. Hili linadhihirishwa na mafanikio ya simu maalumu za ‘Smartphone’ za ‘Ascend Y200’ ambazo zimekuwa suluhisho kubwa katika nyanja mbalimbali za mawasilino, ukiongeza na maboresho yaliyofanywa na mtandao Tigo wa kuongeza spidi ya Intaneti hadi kufikia kiwango cha juu cha 42mbps, tunasisitiza kuwa simu mpya aina ya ‘Ascend Y300 ndio chaguo bora kabisa ambayo wateja wetu wapendwa wanaweza kujivunia.
Simu hizi mpya na maalumu kabisa za Ascend Y 300 zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima kwa bei poa kabisa ya Tsh 195,000/- tu. Pia, wateja watakaonunua simu hizi watafurahia huduma ya Smartpack bure ambayo itawawezesha kupata huduma za Intaneti bila kikomo na bonasi ya muda wa hewani wa Tsh30,000/- wa kupiga simu bure ndani na nje ya nchi kwenye mtandao wowote.
إرسال تعليق