Waasi wa M23 nchini Kongo washutumiwa kwa kulazimisha raia wakiwemo watoto kuingia katika mapigano.


YOUNG m23
Waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidekrasi ya Kongo wamelaumiwa kwa kuwalazimisha raia wakiwemo watoto kujiunga na mapambano mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (MUNUSCO).
Taarifa hiyo imetolewa wakati kikosi maalum cha Umoja wa Afrika kimetumwa Kongo kuyanyang’anya silaka makundi ya wapiganaji.
Msemaji wa kijeshi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa (MUNUSCO) Kanali Prosper Basse ameviambia vyombo vya habari kuwa waasi wa M23 wamekuwa wakilazimisha raia wanaoishi katika wilaya ya Ruchuro unayodhibitiwa na waasi hao, kufanya doria katika misafara pamoja na wapiganaji wao kila siku na kuendelea kuongeza watu ikiwemo watoto.

Post a Comment

Previous Post Next Post