Waasi
wa M23 katika Jamhuri ya Kidekrasi ya Kongo wamelaumiwa kwa
kuwalazimisha raia wakiwemo watoto kujiunga na mapambano mashariki mwa
nchi hiyo.
Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (MUNUSCO).
Taarifa hiyo imetolewa wakati kikosi maalum cha Umoja wa Afrika kimetumwa Kongo kuyanyang’anya silaka makundi ya wapiganaji.
Msemaji
wa kijeshi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa (MUNUSCO) Kanali Prosper Basse
ameviambia vyombo vya habari kuwa waasi wa M23 wamekuwa wakilazimisha
raia wanaoishi katika wilaya ya Ruchuro unayodhibitiwa na waasi hao,
kufanya doria katika misafara pamoja na wapiganaji wao kila siku na
kuendelea kuongeza watu ikiwemo watoto.
إرسال تعليق