Wabunge Wakutwa kwenye Danguro la Uchi Dodoma

 Watu wanaingia mmoja mmoja, wengine kwa makundi na baadhi wapo nje wakipunga kwanza upepo kabla ya kuingia.

Siku hizi wanawake wanaingia bure au kwa jina jingine ‘ladies free’ jambo linalosababisha ukumbi huu ufurike watu.

Katika ukumbi huu, yapo maeneo mawili. Kuna sehemu ya kawaida ambayo kiingilio chake ni kuanzia Sh5,000 hadi Sh10,000 kutegemeana na matukio au burudani ya siku hiyo.

Pia kuna eneo jingine ambalo ni kwa watu maalumu ama waweza kusema ni ‘VIP’ ambapo wateja wake hutakiwa kulipa Sh20,000.

Ukumbi wa VIP upo juu na ule wa kawaida upo chini. Hata hivyo maeneo yote haya hujaza watu kwa kiasi kikubwa.

Mwandishi wetu alifika katika ukumbi wa VIP saa tano usiku, hata hivyo bado watu ni wachache katika eneo hili ukilinganisha na kule kwa watu wa kawaida.

Ukumbi wa VIP si mkubwa kieneo . Kuna kaunta ya vinywaji, makochi madogo madogo aina ya sofa yenye meza mbele yake, viti vilivyoizunguka kaunta na katikati ya ukumbi huu kuna meza mbili za duara zenye mti wa chuma katikati.

Kadri dakika zinavyojongea, ndivyo watu wanavyoendelea kumiminika mmoja baada ya mwingine.

Saa saba za usiku ndipo Mwandishi wetu  aliposhuhudia kiongozi mmoja wa kitaifa ambaye hekima zake zinategemewa na Serikali na hata chama chake akiingia katika ukumbi huu akiwa na mabinti wadogo watatu.

Alipata nafasi ya kuketi, katika moja ya sofa zilizokuwa katika ukumbi huo, akaagiza vinywaji na kuendelea kunywa.

Muda wa saa saba, alitokea msichana aliyevaa sidiria na kisketi cha kujimwaga kifupi sana ambacho hata hivyo kiliuonyesha mwili wake waziwazi.

Msichana yule alipanda katika moja ya meza za duara zenye chuma na kuanza kucheza muziki uliosikika katika spika za ukumbi huo.

Baada ya kucheza kwa zaidi ya nusu saa, alivua kisketi cha rangi nyeusi alichokivaa na kukirusha… akabaki na nguo ya ndani aina ya ‘bikini’ ya rangi nyeupe, kisha akaendelea kucheza kwa kupandia vyuma katika meza hizo za duara.

Baadaye alivua sidiria, akaendelea kucheza na kadri watu walivyokuwa wakimtunza fedha aliendelea kuonyesha ujuzi wake katika kucheza.

Baada ya muziki huo kukolea, msichana huyo alibadilisha mchezo, akalala kifudifudi na kuishusha nguo yake ya ndani hadi nusu ya makalio yake.

Wanasiasa waliokuwepo katika ukumbi huo pamoja na watu wengine walionekana kumpa fedha kwa kumwekea katikati ya makalio msichana huyo kadri walivyofurahishwa na uchezaji wake.

Wakati huohuo mwanasiasa mwingine kijana aliingia ukumbini hapo akiwa na rafiki zake na kuendelea kushuhudia dansi hiyo.

Baada ya kucheza kwa saa kadhaa, msichana yule alishuka katika meza, kisha akapanda msichana mwingine na kuendelea kucheza.

Aliposhuka, aliingia katika choo cha wanawake na kurudi akiwa amevaa suruali aina ya jeans na tisheti. Wanaume waliokuwa eneo hilo walimwita na kumpongeza, huku wakimnong’oneza maneno ambayo…yalikuwa siri yao.

Chanzo chetu cha habari kinaeleza kuwa wasichana hao ni raia wa Kenya ambao wanadaiwa kuwapo nchini kwa ajili ya kucheza dansi za aina hiyo.

“Wanafanya kazi ya kuhudumia wateja hapo kaunta, lakini unapofika wakati wa kucheza wanacheza,” kinasema chanzo hicho.

Kinaeleza kuwa pamoja na kulipwa kiasi cha fedha kama mshahara na wamiliki wa ukumbi huo, wasichana hao wanajipatia fedha wanazotunzwa wakati wa kucheza.

Chanzo kingine cha habari kinaeleza kuwa wasichana hao ni muunganiko au jumuiya ya vijana waliotoka nchi jirani kuja kufanya biashara hiyo ambayo imeshamiri nchini mwao.

Chanzo hicho kinaeleza kuwa, si wanasiasa hao waliokuwapo siku hiyo pekee, bali wanasiasa wa kiume kadhaa wenye majina nchini hufika hapo kutazama wanawake wachezao utupu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Hassan Ngwilizi, Mbunge wa Mlalo (CCM) anasema kwa kuwa wamefanya jambo hilo nje ya Ukumbi wa Bunge hivyo, hawastahili kuhukumiwa bali sheria inatakiwa kuwabana kama wananchi wa kawaida.

Hata hivyo, anasema kitendo hicho ni kinyume cha maadili na hakitakiwi kufanywa na viongozi kama hao.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe anasema sheria za nchi haziruhusu kumbi za starehe kuajiri watu wanaocheza utupu. Waziri Chikawe ambaye pia ni Mbunge wa Nachingwea anasema ni aibu kwa viongozi kutazama dansi za namna hiyo na baya zaidi kuwatuza fedha wachezaji.

“Wanapowatunza fedha, ni kama wanasifia hicho kitendo, ni kama wanasema hivi ndivyo inavyotakiwa” anasema Chikawe na kuongeza:

“Hata hivyo, wanapata wapi leseni za kuendesha huduma kama hizo?”

Anasema Tanzania ni nchi inayozingatia maadili ndiyo maana siku za karibuni Bunge lilipiga marufuku ‘kanga moko’ licha ya hao wacheza utupu.

Anaongeza: “Viongozi wanaotakiwa kuwa mfano wa kuigwa wanapoangalia dansi hizo, wanaendelea kumong’onyoa maadili”

Waziri Chikawe aliahidi kuzungumza na naibu wake, Angela Kairuki ili kuchukua hatua stahiki kwa klabu zinazoruhusu wasichana kucheza uchi.


Mwananchi
Katika ukumbi maarufu wa muziki au kwa jina jingine ‘club’ (jina linahifadhiwa) uliopo mjini  Dodoma mengi yanatokea.

Post a Comment

أحدث أقدم