
Wananchi
wa Afrika Kusini wamekesha wakimuombea afya njema rais wa zamani wa
nchi hiyo mzee Nelson Mandela nje ya nyumba yake ya zamani katika
kitongoji cha Soweto.
Kundi
kubwa la wananchi hao ilikuwa ikiimba na kumuomba Mwenyezi Mungu ampe
nafuu Mzee Mandela, ambaye amelazwa kwa 20 katika hospitali mjini
Pretoria na hali yake imeelezwa kuwa mbaya lakini imara.
Rais
Jacob Zuma wan chi hiyo amemtembelea Mzee Mandela mwenye umri wa miaka
94 na kueleza kuwa hali yake imeanza kuimarika lakini bado yu
mahututi.Rais Zuma ameahirisha ziara yake nchini Msumbiji ambako
angehudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
إرسال تعليق