Mengi kama haya tumekuwa tukiyasikia tukiyasikia yakitokea katika nchi
zilizo bara la America na Ulaya, lakini sasa yameanza kutokea kwa nguvu zaidi
katika bara letu lenye utamaduni wa kipekee na safi (Afrika) watu
wanaojihusisha na mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja wameanza kupaza sauti
hadharani kuomba vitendo vyao vipewe baraka na vyombo vya dola.
Huko nchini Afrika kusini wanawake wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja
(Lesbians) wamejitokeza hadharani kupinga sera za serikali ambazo hazizitambui
haki zao wanazodai kuwa ni za msingi. Moja kati ya madai yao ni kutaka haki ya
ndoa ya jinsia moja kuhalalishwa na pia waweze kurusiwa kuwa na wapenzi wao wa
jinsia moja hadharani kama ilivyo kwa mapenzi tuliyozoea Africa kati ya watu wa
jinsia tofauti.
Sera mapenzi ya jinsia moja lilianza kuwekwa hadharani na nchi za Ulaya kama
Uingereza kwa kutaka kushinikiza nchi
za Afrika kubariki swala la ushoga la sivyo Uingereza itasitisha misaada kwa
nchi zitakazopinga.
Eeeh Mungu tuepushe na hii hali, njaa ya misaada isitupeleke shimoni.
Eeeh Mungu tuepushe na hii hali, njaa ya misaada isitupeleke shimoni.
إرسال تعليق