Juma Seif Kijiko aliyesajiliwa Ruvu Shooting Stars |
KIUNGO wa zamani wa Yanga aliyekuwa akiichezea African Lyon katika Ligi Kuu iliyoisha hivi karibuni, Juma Seif Dion 'Kijiko' ametua Ruvu Shooting kwa mkataba wa miaka miwili.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, Kijiko alisaini mkataba huo jana tayari kuichezea timu yao kwa msimu ujao.
Bwire alisema Kijiko anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na timu yao baada ya kuwanyakua Cosmas Ader kutoka Azam, Elias Maguli (Prisons-Mbeya), Juna Nade (Kagera Sugar) na Jerome Lembeli toka Ashanti United.
Aidha Bwire alisema klabu yao imewatema kikosini wachezaji watano kwa sababu mbalimbali ikiwemo kushuka viwango na kuwataja kuwa ni Paul Ndauka, Charles Nobert, Gido Chawala, Frank Mabande na Liberatus Manyasi.
"Tumemsajili kiungo wa zamani wa Yanga, Juma Kijiko aliyeichezea Lyon msimu uliopita na pia tumewaacha wachezaji wetu watano kwa sababu mbalimbali na kikosi chertu kitaanza kujifua kwa msimu ujao kuanzia Juni 24," alisema Bwire.
Bwire aliwataka wachezaji wote wa timu hiyo kuhudhuria mazoezi hayo yatakayokuwa chini ya kocha wao Charles Boniface Mkwasa
إرسال تعليق