Watu 37 wafariki kwenye machimbo CAR

CAR ina rasilimali nyingi ya madini
Wachimba migodi 37 wameuawa baada ya mvua kubwa kusababisha kuporomoka kwa machimbo walimokuwa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Maafisa wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea Jumapili karibu na mji wa Ndassima, umbali wa kilomita 440 Mashariki mwa mji mkuu,Bangui.

Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ina utajiri wa dhahabu na almasi lakini imekumbwa na mzozo wa muda mrefu, baada ya waasi kupindua serikali mwezi Machi.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, siku tatu za kuomboleza zimetangazwa nchini humo.
Msemaji wa rais Prosper Ndouba, alisema kuwa anahofia kuwa watu zaidi huenda wakafariki.
"kufikia sasa idadi ya waliofariki ni 37, ingawa kuna wengi zaidi waliojeruhiwa, '' alisema bwana Ndouba
Afisaa mmoja ambaye hakutajwa jina aliambia shirika la habari la AFP kuwa idadi kubwa ya wachimbaji walikuwa kwenye machimbo hayo yaliyogeuka na kuwa tope baada ya mvua kubwa kunyesha na hivyo kuwaporomokea.

Post a Comment

أحدث أقدم