Na John Banda, Dodoma.
KUFUATIA kauli iliyotolewa na mbunge wa kilindi Beatrice
Shelekindo ya kuwa msikiti wa barabara ya saba uliopo katika manispaa ya Dodoma unafundisha mafunzo
ya ugaidi na kareti kwa waumini wake imeuathiri msikiti huo.
Akizungumza na Jombo Shekhe Mohamed Awadhi wa msikiti huo
alisema kauli yake hiyo Imeuhathiri waumini wake kutokana kuukimbia na baadhi
ya wanafunzi waliokuwa wakisoma masomo kuhamishwa na wazazi wao.
Awadhi
alisema hivi sasa wapo katika wakati mgumu kutokana na waumini
waliokuwa wakiswali ndani ya msikiti huo kuamua kuhama baada ya kutolewa
kauli ambayo wanaamini ni ya uzushi na uchochezi kwa ajili ya kupotosha
jamii na
serikali.
Shekhe huyo alisema kuwa msikiti huo umejengwa kwa miaka mingi na karibu
baadhi ya wanaoswali ni pamoja na viongozi wa kiserikali wakiwemo askari toka
taasisi mbalimbali kama vile polisi,wanajeshi,usalama na takukuru.
“Sasa kama kweli sisi tungekuwa tunafundisha hayo mafunzo ya
ugaidi na kareti,serikali pamoja na waumini kutoka vyombo vya dola kweli msikiti
huo ungeachwa bila kuchukuliwa hatua zozote”aliuliza Shekhe Awadhi.
Naye mlezi wa wanafunzi wa msikiti huo wa barabara ya saba Husseni
Hamedi Fundi,alikiri baadhi ya wazazi na walezi kuwahamisha watoto wao kutokana
na kauli iliyotolewa na mbunge huyo wa jimbo la Kilindi.
Fundi alisema kuwa msikiti unapokea wanafunzi kutoka nje ya Mkoa
wa Dodoma kama vile Kigoma,Singida,Mwanza,Pemba, Zanzibar,Tanga na Bukoba kwa
ajili ya kujifunza lugha ya kiarabu na elimu ya
Quran.
“Lakini hivi sasa baadhi yao wamehamishwa na wazazi, walezi hii
yote ni kutokana na uzushi uliotolewa na Mbunge huyo wa Kilindi ambaye sisi
kama waumini wa msikiti huo tunaona amepotosha jamii na serikali yetu,
''Kutokana na kauli yake hiyo imetudhalilisha sana hivyo tunaamini Mwanamama huyo anatakiwa
kusema ukweli ukizingatia kuwa sehemu anayoielezea ni Bunge ambalo
linalotengemewa na Watanzania wote'', Alisema Fundi
Kauli hiyo iliyoleta utata ilitolewa na Mbunge wa jimbo la
Kilindi Beatrice Shelukindo mei 4, mwaka huu wakati akichangia bajeti
ya Wizara ya mambo ya ndani alisema msikiti huo wa barabara ya saba unatoa
mafunzo ya ugaidi na kareti.
Mwisho
إرسال تعليق