Timu ya Young Africans inatarajiwa kwenda kanda ya Ziwa mwishoni mwa wiki ijayo kwa ajili ya kucheza michezo ya kirafiki ya kujiandaa na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu 2013/2014, ambapo itatumia fursa hiyo kuwaonyesha kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom na kusherehekea pamoja na wpenzi, washabiki na wanachama wake.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, mkurugenzi wa kampuni ya Nationwide ambao ndio waandaji wa ziara hiyo Frank Pangani amesema wao wanatumi afurs ahiyo kwa wakazi wa kanda ya ziwa kupata fursa ya kuwaona wachezaji wa Yanga wakiwa na kombe lao la Ubingwa wa Vodacom pamoja na kushuhudia michezo ya kirafiki ya kimataifa.
Naye Afisa Habari wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto amesema ziara hiyo wataitumia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom, wanachama na wapenzi wa Yanga kuliona kombe la Ubingwa ikiwa ni pamoja na kucheza michezo ya kirafiki ambayo mwalimu ataitumia kwa ajili ya kukiandaa kikosi chake.
Ziara ya Mabingwa au Champions Tour ni tukio la kila mwaka linalowahusishwa mabingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mabingwa wa soka waalikwa wa kutoka nchi jirani za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na pia timu alikwa ya nyumbani.
Mara ya kwanza tukio hili lilifanyika mwaka jana 2012, kwa bingwa wa Tanzania Bara wa msimu uliopita, timu ya Simba Sports Club (SSC) ya Dar Es Salaam kushiriki ziara hiyo kucheza na mabingwa wa Uganda wa msimu uliopita timu ya The Express ya Kampala na Toto African ya Mwanza.
Mwaka jana 2012 ziara hiyo ya mabingwa ilifanyika katika mikoa ya Mwanza (Uwanja wa CCM Kirumba), Simba ilicheza na Toto African ya Mwanza, Shinyanga (Uwanja wa CCM Kambarage) Simba vs Express, na Dar Es Salaam (Uwanja wa Taifa) Yanga vs Express na Simba vs Express.
Mwaka huu 2013 itakuwa ni mara ya pili kwa tukio hili la Ziara ya Mabingwa kufanyika chini ya uandalizi wa taasisi ya michezo ya Natiowide Entertaiment Centre (NEC) yenye makao yake jijini Mwanza.
Ziara ya Mabingwa mwaka huu wa 2013 itawahusisha mabingwa wa Tanzania Bara, Young Africans Sports Club (YASC) ya Dar Es Salaam na waalikwa mabingwa wa mwaka huu wa Uganda timu kongwe na mashuhuri ya Kampala City Council (KCC) ya jijini Kampala na pia timu alikwa ya ndani inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo itatangazwa ndani ya muda wa siku mbili kutoka leo.
Mechi za Ziara ya Mabingwa mwaka huu wa 2013 zitachezhwa katika mikoa ya Mwanza (CCM Kirumba) Jumamosi 06/07/2013 Yanga vs KCC, Shinyanga (CCM Kambarage) Jumapili 07/07/2013 Yanga vs KCC marudiano, na Tabora (Ali Hassan Mwinyi) Alhamisi 11/07/2013 Yanga vs timu ya nyumbani itakayotangazwa siku mbili zijazo. Baada ya mechi hizo ziara hiyo inatarajiwa kuendelea katika mikoa itakayotanagazwa baadae.
Nationwide Entertainment Centre pia inazishukuru timu zote zinazoshiriki ziara hii ya mabingwa kila mwaka wakiwemo mabingwa wa msimu huu Yanga na mabingwa wa msimu uliopita watani wao wa jadi Simba ambao wametoa ushirikiano mkubwa, na wadhamini wa mwaka huu Kilimanjaro Premium Lager na vyombo vya habari.
إرسال تعليق