Salaam.Tanzania
WAKATI wanafunzi wa kidato cha nne waliokuwa wamefeli katika mitihani
yao ya mwaka jana wakifaulu kwa alama nyingi baada ya alama za ufaulu
kurekebishwa, Baraza la Mitihani Nchini (Necta), limetangaza matokeo ya
kidato cha sita ambapo asilimia 87.85 wamefaulu huku kundi la shule 20
za mwisho likitawaliwa na shule kongwe nchini na zile za Zanzibar.
Imekuwa ni kawaida kwa Shule za Zanzibar kufanya vibaya katika
mitihani ya Taifa nchini Tanzania zikifuatiwa na Shule Kongwe za
Serikali.
Akitangaza matokeo hayo jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo,
Dk Charles Msonde, alisema watahiniwa 50,611 walifanya mtihani huo na
kati yao 44,366 sawa na asilimia 87.85, wamefaulu.
Mwaka 2012 wanafunzi waliofaulu mtihani huo walikuwa ni 46,658 sawa na asilimia 87.65. Watahiniwa wa shule Dk Msonde alisema kuwa, watahiniwa wa shule waliofaulu ni 40,242 sawa na asilimia 93.92 ya waliofanya mtihani huo.
“Wasichana waliofaulu ni 13,286 sawa na asilimia 95.80 na wavulana 26,956 sawa na asilimia 93.03,” alisema. Mwaka 2012 watahiniwa 40,775 sawa na asilimia 92.30 walifaulu mtihani huo. Watahiniwa wa kujitegemea Alisema kuwa, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo walikuwa ni 7,659 na waliofaulu ni 4,124 sawa na asilimia 53.87.
Ufaulu katika kundi hili umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo
watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 5,883 sawa na asilimia 64.96 ya wote
waliofanya mitihani hiyo. Ufaulu kwa madaraja Matokeo
hayo yanaonyesha kuwa, watahiniwa 325 sawa na asilimia 0.76 ya wote
waliofanya mtihani huo walipata daraja la kwanza, kati yao wavulana
wakiwa ni 188 sawa na asilimia 0.65 na wasichana 137 sawa na asilimia
0.99.
إرسال تعليق