Zitto Kabwe amefunguka na kudai kuwa kwa sasa wanajiandaa kufanya mapinduzi ya nchi endapo serikali watu walioficha mabilioni uswiswi hawatashughulikiwa ipasavyo....
Suala la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.
Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge.
Zitto Kabwe anatoa angalizo katika hatua hiyo ya jaji Werema kwa kusema kuwa hatua hii isiwe "zima moto" na daganya toto ili kuwafumba macho watanzania...
Ubabaishaji wowote kwa mujibu wa Zitto Kabwe utasababisha mapinduzi ya nchi.....
Hii ni post yake aliyoweka katika mtandao wa twitter
إرسال تعليق