Balozi Liberata Mulamula akishuka kwenye gari Bethesda, Maryland
wakati akitokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling,
Virginia Ijumaa July 12, 2013. Mhe, Mulamula ndiye Balozi wa Tanzania
nchini Marekani aliyekuja kuchukua nafasi ya Balozi Mwanaidi Maajar
aliyemaliza muda wake mwanzoni mwa mwaka huu. Kabla ya hapo Balozi
Mulamula alikua Balozi wa maziwa makuu na msaidizi wa Rais mwandamizi
katika maswala ya diplomasia.
Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Maafisa na Wafanyakazi wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliofika kumlaki kwenye yatakayokua
makazi yake Bethesda, Maryland.
Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Maafisa na Wafanyakazi wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliofika kumlaki kwenye yatakayokua
makazi yake Bethesda, Maryland.
Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Maafisa na Wafanyakazi wa
Ubalozi (hawapo pichani) wakati walipomkaribisha nyumbani kwake,
Bethesda, Maryland.
Watoto wa Mhe. Balozi Alvin na Tanya.
Mume wa Mhe. Balozi, Bwn. George Mulamula.
Kaimu Balozi na mkuu wa Utawala na Fedha, Mama Lily Munanka katika picha.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akibadlishana mawili matatu na Maafisa
na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakati
walipomkaribisha nyumbani kwake Bethesda, Maryland kushoto ni Afisa
Ubalozi Mindi Kasiga.
Juu na chini ni Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani wakiwa tayari kumpokea Mhe. Balozi Mulamula na familia yake.
إرسال تعليق