![]() |
| Hajatulia: Lakini vigogo wa Katalunya, Barcelona wanamtaka Wayne Rooney kuongeza mtu wa nguvu katika safu yao ya ushambuliaji |
KLABU ya Barcelona inataka kuwatoa
Thiago Alcantara na David Villa sambamba na kiasi fulani cha fedha Old
Trafford ili wapewe Wayne Rooney akacheze Hispania.
Vigogo hao wa Katalunya wanataka
kuimarisha safu yao ya ushambuliaji licha ya kwamba tayari wanaye Neymar
waliyemsajili mwezi uliopita.
Rooney, ambaye aliishuhudia Fainali ya
michuano ya Tenisi ya Wimbledon jana Andy Murray akitwaa taji upande wa
wanaume, anakabiliwa na kiza juu ya mustakabali wake Manchester United
na aliomba kuondoka mwishoni mwa msimu.
Mlengwa: Dili la Rooney litafanya United imsaini Thiago Alcantara, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford
Arsenal na Chelsea bado wana matumaini
ya kumnasa mshambuliaji huyo wa England ahamie London, ingawa ukweli
unabaki hilo litakuwa jambo gumu kwa United kuwauzia silaha wapinzani.
Rooney na David Moyes wamekwishazungumza
juu ya mustakabali wake: wawili hao walikutana nyumbani kwa Rooney
kabla hata wachezaji hawajarejea kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu
mpya wiki iliyopita, na Mscotland huyo akaweka wazi katika Mkutano wake
wa kwanza na Waandishi wa Habari wiki iliyopita.
Kocha huyo mpya wa United anatarajiwa
kutoa taarifa yake ya usajili baada ya kurithi mikoba ya Sir Alex
Ferguson rasmi mapema mwezi huu.
Mshambuliaji mpya: United pia itanufaika na David Villa katika dili hilo - ambaye pia anatakiwa na Tottenham
Kocha mpya: David Moyes anataka kuweka alama yake United baada ya kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson
Na hiyo imelifanya gazeti la Sport la Hispania kuandika kwamba Rooney anaweza kutumika kuongeza ubora La Liga.
Taarifa katika gazeti hilo imesema
kuondoka kwa Thiago kwa kiasi cha Pauni Milioni 17 ni kama kunawezekana
na zaidi katika dili hilo, Villa pia, mwenye thamani ya Pauni milioni
8.5 ataondoka Nou Camp akiwa amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake.
Pamoja na hayo, Pauni Milioni 4 taslimu itaongezwa ili kufikisha tahamani ya Rooney, zaidi ya Pauni Milioni 30.
Suti na buti: Rooney alikuwa eneo la
watu mashuhuri, maarufu kama Royal Box akiangalia Andy Murray akitwaa
taji la Wimbledon jana

Beki, na mchezaji wa zamani wa United,
Gerard Pique alimpamba sana mchezaji mwenzake huyo wa zamani wiki
iliyopita kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atakuwa mmoja
wa wachezaji bora duniani akihamia Barca.

إرسال تعليق