![]() |
| Wote wanatabasamu: Edinson Cavani akiondoka katika hospitali ya Pitie Salpetriere baada ya kufanyiwa vipimo kuelekea kujiunga na PSG |
MSHAMBULIAJI Edinson Cavani yuko katika hatua za mwishoni za kutua Paris St Germain kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 55.
Muuwaji huyo wa Uruguy atajiunga na klabu hiyo akitokea Napoli ya Italia baada ya kukataa kuhamia Ligi Kuu ya England.
Manchester City na Chelsea zote zilikuwa zinataka kumsajili mchezaji huyo lakini ameamua kwenda Ufarasa.
Cavani
alitua katika ardhi ya Paris Jumatatu na alionekana akiondoka katika
hospitali ya Pitie Salpetriere baada ya kukamilisha vipimo.
Mabingwa hao wa Ufaransa watafanya Mkutano na Waandishi wa Habari Jumanne kwa ajili ya kumtambulisha mchezaji wao huyo mpya.
Habari hizi zitakuwa pigo kubwa kwa timu za Ligi Kuu ya England.

Mvuto wa nyota: Cavani akiwapungia mashabiki nchini Ufaransa baada ya kukamilisha vipimo vya afya
Kocha
wa Chelsea, Jose Mourinho anataka kuongeza mshambuliaji na mustakabali
wa Fernando Torres na Demba Ba upo shakani katika klabu hiyo.
City,
wakati huo huo, imewapoteza Carlos Tevez na Mario Balotelli katika
miezi ya karibuni na kubaki na Sergio Aguero na Edin Dzeko katika safu
ya ushambuliaji.

إرسال تعليق