Mh. Kalley Pandukizi
Kikao cha Viongozi wa Tawi la Chadema Washington DC,
Marekani, tarehe 27 July 2013 kimemteua
Ndugu Kalley Ammy Pandukizi kuwa
Mwenyekiti wa Tawi kuchukua nafasi ya Ndugu Cosmas Wambura. Awali Ndugu Kalley
Pandukizi alikuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tawi la Chadema DMV linalobeba
majimbo matatu ya Washington DC,
Maryland na Virginia. Baadae alikuwa Afisa wa Habari wa Tawi na nafasi yake
kuchukuliwa na Cosmas Wambura. Viongozi wengine na nafasi zao ni Katibu wa Tawi
ni Libearatus Mwang’ombe aliyekuwa katibu wa kwanza wa Tawi, aliyechukua nafasi
ya Isidory Lyamuya. Katibu Mwenezi
ni Ndugu Hussein Kauzela na Mweka
hazina ni Ndugu Ludigo Mhagama. Mwenyekiti
wa Baraza la wanawake ni Ndugu Baybe
Mgaza na Katibu wa Baraza la wanawake ni Mariam Khamis. Nafasi nyingine ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Ndugu
Amri Maliyatabu na katibu wa baraza
la vijana ni Ndugu Stephen Msungu. Nafasi nyingine ni
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee ni Amos
Cherehani na Katibu wa baraza la wazee ni Elias Mshana. Nafasi ya Mwisho ni ya Baraza la Washauri
linaloongozwa na Prof Nicolas Boaz
na Emmanuel Muganda.
Akizungumza baada ya Uteuzi huo Mwenyekiti wa
Chadema Washington DC Ndugu Kalley,
Amewashukuru Viongozi wote kwa kumwamini na kumpa nafasi hiyo kwa mara ya pili
na kuwaahidi kufanya mambo makubwa ikiwemo kurudisha uhai wa Tawi na
kuwaunganisha wanachama kuwa wamoja. Pia ameahidi kushirikiana na Jumuia
nyingine ikiwemo Jumuia ya Watanzania DMV, Ofisi ya Ubalozi Wa Tanzania
Marekani, Jumuia ya Waislam waishio Washington DC (TAMKO) na Uongozi wa CCM DMV ili kujenga Tanzania Moja
yenye mshikamano.
Pia Ndugu Kalley
amesema baada ya kurudi kwenye
nafasi hiyo kipaumbele cha kwanza kitakuwa kuvalia njuga mambo makuu mawili
ambayo ni Suala la mchakato wa Katiba unaoendelea ili kuhakikisha kuwa Tanzania
inapata Katiba nzuri iliyoridhiwa na Watanzania wote bila kuingiliwa na mtu
yeyote kwa nia mbaya. Pili amesema atavalia njuga suala la upatikanaji wa Tume
huru ya Uchaguzi ili Uchaguzi Ujao wa Mwaka 2015 uwe huru na Haki.
Aidha Katika mkutano huo Ndugu Kalley ameelezea
kusikitishwa sana na vitendo vya ukiukwaji wa Sheria vinavyofanywa na Jeshi la
Polisi kwa kuwabambikizia kesi raia wasio na hatia na hata matukio ya mauaji
wanayotuhumiwa baadhi ya Askari Polisi. Ndugu Kalley amesema atapambana vikali kuhakikisha matukio hayo ya
ukiukwaji wa haki za raia yanayofanywa na baadhi ya askari Polisi yanakomeshwa,
kwani hakuna sheria inayoruhusu askari Polisi kujichukulia sheria mkononi
wakati Mahakama ndizo zilizopewa Mamlaka hiyo.
Tawi la Chadema Washington DC lilianzishwa rasmi tarehe 26 Aprili 2012 chini ya usimamizi wa Mbunge wa viti maalum Mh Leticia Nyerere na Kufunguliwa rasmi tarehe 27 Mei 2012 na Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu katibu mkuu wa Chadema Mh Zitto Kabwe. Sherehe hizo za Ufunguzi ziliudhuriwa Pia na Mbunge wa Iringa mjini Mh Peter Msigwa, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari, Mbunge wa Viti Maalum Kwimba Mh Leticia Nyerere na Mbunge wa Viti maalum Kutoka Zanzibar Mh Mariam Msabaha.
إرسال تعليق