Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimetangaza kutomtambua msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa na kusema wao walishamfuta kabla ya yeye hajakifuta chama hicho.jamiiforums
Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr. Willbroad Slaa amesema wao hawatishwi na kauli ya msajili John Tendwa ya kukifuta chama hicho maana wao wanaitambua ofisi ya msajili wa vyama vya siasa tu na si John Tendwa.
Amezungumza hayo hii leo jijini Dsm wakati wa uzinduzi wa kongamano la kimataifa la vijana kuhusu demokrasia.
إرسال تعليق