Kwa mara ya kwanza msanii wa kike Recho kutoka THT alipoanza kutoa nyimbo na kusikika, hisia za watu wengi ziliemwendea msanii wa kike Ray C
aliyejipatia umaarufu hapa nchini kutokana na uimbaji wake na hususan
‘viuno vyake’ awapo jukwaaji, sababu kubwa ikiwa ni Recho amefanana sana
na Ray C sauti, uimbaji, uchezaji wa jukwaani pamoja na muonekano.
Kitu ambacho huenda wengi tulikuwa hatufahamu ni mtazamo wa Ray C
juu ya Recho ambaye ni kama mdogo wake kiumri na hata kimuziki hasa
kuhusu maoni ya watu wanaosema kua ana mcopy.
Leo (July 22) Ray C ametoa jibu la swali hilo baada ya kupost picha
ya Recho (akiwa jukwaani) katika akaunti yake ya Instagram. Baada ya
picha hiyo ambayo ilikuwa haina caption mashabiki walianza kutiririka
kwa maswali ambayo yalisaidia Ray C kutoa hisia zake juu ya Recho
aliyemuita dogo lake. Ray aliandika “Dogo Langu
Kazini,kwasababu ananipenda na kunikubali lazma tutaimba wote wimbo
mmoja for You guys cz hata mimi penda sauti yake sana!!!!!! Miss
Upepo@rachelkizunguzungu”.

Picha ya Recho aliyoipost Ray C
Shabiki mmoja alimuuliza swali Ray C ”getmoo1:Uko tofauti ray c
thought ungechukia dogo kukucopy ..she is fine ila copy and paste but
huo u regendary..sema ttz mtu akiku copy then akudis”.
Na jibu la Ray C lilionesha kuwa Rehema hana tatizo kabisa na swala la Recho kumcopy “Am happy tht am her @getmoo1 Role Model nafurahi kumuhamasisha nae kuingia kwenye music industry”.
Na jibu la Ray C lilionesha kuwa Rehema hana tatizo kabisa na swala la Recho kumcopy “Am happy tht am her @getmoo1 Role Model nafurahi kumuhamasisha nae kuingia kwenye music industry”.
Recho ambaye alianza kufahamika zaidi kupitia wimbo wake wa
‘Kizunguzungu’ alikuja kipindi ambacho Ray C alikuwa amekaa kimya sana
hivyo uwepo wake uliwafariji mashabiki wa Ray C waliovikosa viuno vyake
vya jukwaani na sauti yake iliyotawala katika chati za bongo flevah
miaka kadhaa iliyopita.
Unahisi wasanii hawa wawili wanaofanana kuanzia herufi za mwanzo za
majina yao ‘R’, sauti, uimbaji na hata uzungushaji wa viuno jukwaani,
wakikaa katika wimbo mmoja itazaa kitu gani? Na ikitokea Collabo hiyo ya
Ray C na Recho kwa jinsi unavyowafahamu unahisi nani atamfunika
mwenzake?

إرسال تعليق