
Mwendesha baiskeli aliyezaliwa
Kenya ingawa raia wa Uingereza Chris Froome, anasema kuwa anatumai
ushindi wake wa mashindano ya Tour de France utaweza kuwapa motisha
vijana wa kiafrika.
Froome alishinda awamu ya miamoja ya mashindano ya Tour De France mnamo Jumapili akiwa anawakilisha Uingereza.Alianza kuingia katika mashindano ya baiskeli baada ya kusaidiwa na mwendesha baiskeli mashuhuri nchini Kenya David Kinjah, na kushinda medali kwenye mashindano ya Afrika mwaka 2007 kabla ya kuhamia Uingereza.
Alienda shuleni nchini Afrika Kusini.
Baada ya kushinda mashindano hayo, alisema ushindi wake unalenga kuwapa matumaini vijana hususan vijana wa kiafrika.
''Lazima waamini kuwa wanaweza kutoka nje ya bara la Afrika kuweza kujiunga na vikosi vya Ulaya,'' alisema Froome
Alishinda kwa zaidi ya dakika nne huku akishikana mikono na wenzake wa kikosi cha Uingereza.
إرسال تعليق