GARI LA WAKILI ALIYETISHIA KUMUUA TRAFIKI, LAFIKISHWA POLISI

Gari la wakili Erasto likiwa kituo cha polisi Tegeta.
Gari hilo kwa nyuma.
GARI aina ya Toyota Mark II Grande lenye namba za usajili T 181 BMM mali ya wakili Erasto Lugenge limefikishwa kituo cha polisi Tegeta. Wakili huyo ambaye gari lake lilipata ajali usiku wa kuamkia jana saa 6:30 usiku maeneo ya Boko - CCM jijini Dar baada ya kuligonga kwa nyuma gari aina ya Toyota Rav 4 lenye namba za usajili T 347 CAR lililokuwa likiendeshwa na James Mushi. Inadaiwa kuwa, baada ya Wakili Erasto kuligonga gari hilo hakutii amri na badala yake alichomoa bastora na kutishia kumpiga risasi askari wa usalama barabarani, Koplo Aman Leon ambaye alikuwa akipima ajali hiyo. Kufuatia kitendo hicho, askari huyo alimnyang'anya bastola wakili na kuifikisha kituo cha polisi Wazo Hill Tegeta. Kwa sasa wakili huyo anashikiliwa na polisi katika kituo cha Wazo Hill.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika na amewatahadhalisha wananchi kutowaingilia polisi katika utendaji wao wa kazi bali wawape ushirikiano.
(Picha na Makongoro Oging' / GPL)

Post a Comment

Previous Post Next Post