Kampuni
ya Apple watengenezaji wa simu aina ya iPhone imesema itafanya
uchunguzi juu ya madai ya mwanamke mmoja wa China aliyedaiwa kupoteza
maisha kwa kupigwa shoti wakati akizungumza kwa simu yake ya iPhone
aliyokuwa anaicharge.
Madai hayo yamewasilishwa na msichana kutoka magharibi mwa China Xinjiang, aliyeandika barua kwa mtandao maarufu wa China ‘Sina Weibo’ kuelezea kilichomsibu dada yake mkubwa Ma Ailun aliyekuwa na miaka 23.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, polisi wamethibitisha kifo cha msichana
huyo kimetokana na shoti ya umeme, lakini haijathibitishwa bado kama
simu yake ilihusika.
Msemaji wa Apple nchini China Carolyn Wu amesema wanafanya uchunguzi
juu ya tukio hilo na pia akatoa pole kwa familia ya marehemu. “We will
fully investigate and cooperate with authorities in this matter,”
Alisema

Post a Comment