Hivi ndivyo SwahiliTv ilivyolonga na Meneja wa Justin Bieber “Justin kukaa kifua wazi”

Picture
Katika pitapita zetu mitaa ya Connecticut, Marekani, mwandishi wetu alikutana na picha hizi za Bieber akiwa kifua wazi halafu amejitunisha ili kuonyesha jinsi inavyolipa.

Mwanamuziki huyu mdogo lakini maarufu amekuwa na tabia ya kuvua shati siku hizi hata akiwa klabu au mitaani kwani anasema anataka kinadada waone jinsi kifua chake kilivyo.

Katika kutafuta ukweli wa mambo ilikuweza kuhakikisha je ni kweli amesema hivyo kwa watu, mwandishi wetu wa burudani bwana DMK alimpigia simu meneja wa Justin na kumwuliza lakini yeye alikanusha na kusema bwa'mdogo huyo amekuwa akikaa kifua wazi kwa sababu summer hii joto ni kali sana na mwanamuziki huyo anashindwa kuvumilia. Alipomwomba kuongea na Justin mwenyewe meneja huyo alimkatia simu.

Tutaendelea kufatilia zaidi ili tuweze kupata ukweli je ni kwanini Justin Bieber siku hizi anapenda kukaa kifua wazi? Ama Je!, Ni kwasababu anaenda gymn sana? au?.... endelea kusoma Swahili TV blog na kupitia website yetu www.swahilitv.info
Picture
 

Post a Comment

Previous Post Next Post