Kipindi
cha wiki hii cha Fema Radio Show kimezungumzia biashara ya mapenzi
iliyoshamiri maeneo ya mjini.Katika kipindi hicho, mmoja wa wasichana
wanaofanya kazi hiyo, Aisha amesimulia jinsi alivyoingia kwenye biashara
hiyo baada ya kuvunjika kwa ndoa yake.
“Nilikuwa nimeolewa, niligombana na mume wangu, matatizo tu ya ndani
ya ndoa, kwahiyo nikawa nimerudi nyumbani, pakawa na matatizo, tena
matatizo ya kifamilia, maisha magumu, ndio ikabidi niingie kwenye kazi
hiyo unayoiona,” anasema Aisha.
Aisha anasema mwanzoni alikuwa anajisikia vibaya kufanya kazi hiyo lakini kwa sasa ameshazoea.
“Mimi bado mgeni sijazoeleka, kuna wenyeji wapo wana miaka saba
kwahiyo wanakuwa wameshazoeleka, mtu akipita wanajua wanamuitaje mpaka
mtu anawakubalia kwahiyo inakuwa sio rahisi kwa wewe kupata mtu wa
kwenda naye au kukupa hela.”
“Nachojutia mimi ni kukosa kazi ya kueleweka. Nimejifunza cherehani,
sijaipenda tu kazi ya kushona, sina hobby na ufundi cherehani.”
Post a Comment