Waziri
wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk
akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kimataifa ya huduma za usafiri
ya China (CITS) Zou Wang Sheng (mwenye fulana nyekudu) kushoto ya Sheng
ni Balozi mdogo wa China Madam Chen huko Ofisini kwake Kikwajuni Mjini
Zanzibar.
Picha
no.2 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali
Mbarouk akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Kampuni ya Kimataifa ya huduma
za usafiri ya China (CITS) Zou Wang Sheng baada ya mazungumzo yao huko
Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo
Zanzibar
========= ======== ===========
Na Faki Mjaka-Maelezo
Zanzibar .
Kuokosekana kwa Matangazo ya Vivutio vya
Zanzibar nchini China kumetajwa kuwa sababu inayopelekea Watalii wanaotoka
nchini huko kushindwa kuja Zanzibar kufanya shughuli za Utalii.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kimataifa ya
huduma za usafiri ya China (CITS) Zou Wang Sheng ameyasema hayo katika
mazungumzo yake na Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said
Ali Mbarouk huko Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Sheng amesema China ni miongoni mwa nchi
zinazotoa Wataii wengi kutembelea nchi tofauti duniani lakini Wachina walio
wengi hushindwa kuja Zanzibar kutokana na kukosa taarifa zinazohusu vivutio
hivyo.
Amedai kuwa hata katika Balozi ya Tanzania nchini
China hakuna Matangazo yanayohusu vivutio vya Zanzibar badala yake kunapatikana
Matangazo ya Mbuga za Serengeti na Manyara ambazo zote ziko Tanzania Bara.
Sheng ambaye ni mara yake ya kwanza kuja
Zanzibar ameongeza kuwa kutokana na mazigira mazuri
yakitalii yaliyopo Zanzibar anaamini kama kutafanywa mkakati thabiti
wa kuvitangaza Vivutio vya Zanzibar hapana shaka zaidi ya Watalii 200,000
wanaweza kuitembelea Zanzibar kwa mwaka.
Ameelezea kuvutiwa kwao na Fukwe, hali
ya hewa na mazingira ya Zanzibar kwa ujumla wake na kuahidi atakaporudi
atafanya kazi ya kushawishi makundi ya Wageni kuja kujionea vivutio hivyo. “Tumetembea
nchi nyingi dunia kufanya ziara za kitalii lakini ukweli nikwamba ni nchi
chache sana za visiwa duniani zenye vivutio vizuri kama Zanzibar ” Alisema
Sheng
Awali Waziri wa habari Utamaduni Utalii
na Michezo Said Ali Mbarouk amesema Zanzibar na China zimekuwa na mashirikiano
makubwa kwa muda mrefu hasa katika sekta za elimu, Afya na teknolojia na kwamba
kwa sasa Sekta ya Utalii inapaswa kupewa mkazo wa pekee.
Ameongeza kuwa Zanzibar imekuwa ikipokea
Watalii kutoka nchi nyingi za Ulaya na hasa Wataliano na kwamba umefika muda
sasa walau Theluthi ya Watalii kutoka China kuja kutembelea Zanzibar.
“Taarifa zinaonesha China inatoa Watalii
zaidi ya Milioni moja kwenda kutembelea nchi tofauti duniani sasa tunataka
walau watalii laki tatu watembelee Zanzibar kwa mwaka ” Ameongeza Waziri Mbarouk. Ameongeza kuwa mazingira ya Zanzibar ni
mazuri kwa vivutio vingi vya utalii na hali ya kisiasa ilivyotengamaa na kulitaka
Shirika hilo kufanya jitihada zake ili kuwepo kwa Safari za ndege zinazotoka
China na kuja Zanzibar.
Waziri Mbarouk amewahakikishia
Wawekezaji hao kila aina ya ushirikiano ili kuona Sekta ya Utalii nchini
inasonga mbele kupitia Watalii wa kichina. Kwa upande wake Balozi mdogo wa China
nchini Madam Chen Queman amesema kuwa walipokea ushauri kutoka kwa Rais wa
Zanzibar na Menyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kusaidia
kuitangaza Zanzibar ambapo ujio wa kampuni hiyo ni utekelezaji wa shauri hilo.
Ameongeza kuwa njia pekee ya kufikia
malengo yaliyokusudiwa ni kuhakikisha kunakuwepo mawasiliano na mashirikiano ya
moja kwa moja kati ya Kampuni hiyo na Mamlaka ya Ukuzaji Vitegauchumi Zanzibar
ZIPA.
Madam Chen amesema ZIPA ndio watakao kuwa
Wenyeji wa Kampuni hiyo ili kujua nini kifanyike katika hatua za mwanzo
kuhakikisha Zanzibar inafaidika na Watalii kutoka nchi ya China
إرسال تعليق