Regina
Kumba, HabariLeo — HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imesema hatma ya
jengo la ghorofa 16 lililoko mtaa wa Indira Gandhi na Asia lililoamriwa
kuvunjwa na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka, haijaeleweka kwa sababu Mahakama imeweka zuio la kuvunjwa kwa
jengo hilo.
Akizungumza na gazeti la HabariLeo jana, Msemaji wa manispaa hiyo, Tabu Shaibu alisema kuwa haitawezekana kuvunjwa jengo hilo kwa sasa kwa sababu mmiliki wa jengo hilo, mfanyabiashara Rada Damji amefungua kesi mahakamani kupinga amri aliyopewa ya kuvunja jengo lake.
"Kwa sasa taratibu zote ziko mahakamani, siwezi kusema mahakama gani kwa sababu mwanasheria wetu amesafiri lakini baada ya mmiliki kupewa amri ya kuvunjwa jengo alipinga mahakamani na hivyo kuna zuio la kuvunjwa," alisema Shaibu.
Shaibu alisema Halmashauri ilimtaka mfanyabiashara huyo kuvunja jengo lake baada ya kubainika haliko

salama lakini aligoma na kwamba serikali haiwezi kuingia gharama ya kubomoa jengo ambalo alilijenga yeye.
Waziri Tibaijuka aliitaka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuvunja jengo hilo ikiwa ni siku chache baada ya jengo la ghorofa 16 lililoanguka Machi 29 mwaka huu na kuua watu 36 na wengine kujeruhiwa kwa ajili ya kuepusha maafa zaidi kwa wananchi, kwa kile ilichoelezwa jengo hilo pia lilijengwa chini ya kiwango.
Tibaijuka alimtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutekeleza agizo la kusimamia jengo hilo kuvunjwa ndani ya siku 30 na kama mmiliki atashindwa kutekeleza hilo atozwe faini kwa kila siku hadi uvunjaji utakapokamilika.
Hata hivyo, halikuvunjwa katika muda muo badala yake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema kuwa kazi ya uvunjaji ni nyeti inahitaji muda kutekelezwa na kwamba imeundwa kamati ambayo inafanya utafiti kujiridhisha ubora wake.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Dk Assenga Severine, Manispaa aliajiri wahandisi kutoka Taasisi ya BICO ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyia utafiti jengo lililoamriwa kuvunjwa.
Severine alisema kuwa manispaa yake haina wataalamu hivyo imewalazimu kutafuta wataalamu kutoka nje kwa ajili ya kulichunguza jengo kabla ya kulivunja kama ilivyoagizwa na Waziri Tibaijuka.
Alisema pengine sheria inasema mtu huyo akikiuka anatakiwa kulipa faini na kwamba Manispaa yake itahojiwa kwa nini haikutakiwa kumtaka mmiliki kulipa faini kama sheria inavyotaka na badala yake jengo lote

إرسال تعليق